Jumapili 23 Novemba 2025 - 23:31
Moscow Yafanya Hafla ya Kumbukizi ya Shahada ya Bibi Zahraa (a.s) katika Kituo cha Kiislamu

Hawza/ Hafla ya kila wiki inayofanywa katika Kituo cha Kiislamu nchini Moscow imefanyika sambamba na kuadhimisha siku za Fatimiyya.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, hafla inayofanywa kila wiki na Kituo cha Kiislamu nchini Moscow ilifanyika sambamba na kuadhimisha siku za Fatimiyya. Ratiba hii ilianza baada ya kuswaliwa Magharibi na Isha kwa kisomo cha aya za Qur’ani Tukufu.

Baadaye, Haj Chingiz Ramazanov, ambaye ni mzungumzaji Mrusi wa hafla hiyo, alizungumzia umuhimu wa kuwapa watoto majina mazuri katika utamaduni wa Kiislamu. Akinukuu aya ya 180 ya Surah al-A‘araf: «وَلِلَّهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَیٰ» alisisitiza nafasi ya majina mazuri katika kuleta mazingira ya kimaanawi ndani ya familia. Kisha akarejea riwaya kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) inayosema kuwa nyumba ambayo ndani yake yapo majina kama vile Muhammad, Ali, Hasan, Husayn, Abdullah, Ja‘far na majina yanayofanana, ni nyumba yenye baraka nyingi.

Baada ya hapo, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Mahmud Faqih, akizungumza kwa lugha ya Kiazari, alisisitiza umuhimu wa swala kama nguzo kubwa zaidi ya dini, na akasisitiza ulazima wa kuzingatia hukumu na kufuata kwa uangalifu undani wake.

Aliendelea kuzungumzia nafasi ya Imam Mahdi (a.t.f.s) katika kuwaongoza wanadamu, na akabainisha kuwa; kutawassal kwake na kuswali swala maalumu aliyopendekezewa (rakaa mbili kama swala ya Alfajiri), hasa katika nyakati ngumu, kunaleta utulivu na imani kwa waumini.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Hujjatul-Islam Faqih akasema kuwa; Uislamu ni dini ya kiroho na furaha; hivyo baada ya siku za maombolezo ya Fatimiyya, kwa maadhimisho ya kuzaliwa kwa Bibi Zahraa (a.s) tunaingia katika siku za furaha, kwani kila wakati watu wa nyumba ya Mtume (a.s) wanapofurahi, wafuasi wao pia hufurahi.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alizungumzia utukufu wa Bibi Ummul Banin (a.s), na akabainisha kuwa pamoja na jina lake kuwa “Fatima”, kwa ajili ya kuwafariji watoto wa Bibi Zahraa (a.s) aliomba watu wasimwite kwa jina hilo. Kauli yake maarufu: “Sikuja kuwa mama, bali nimekuja kuhudumia watoto wa Fatima” ni mfano wa hali ya juu wa ikhlasi na kujitolea kwa mwanamke huyu mtukufu. Athari za malezi yake ya kimungu zinaonekana wazi katika tabia ya Bwana Abbas (a.s) na uaminifu wake kwa Imam Husayn (a.s).

Mwishoni wa hafla hiyo, wasomaji wa mashairi ya Ahlul Bayt (a.s) pamoja na waombolezaji walisoma maombolezo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha